Saturday, December 16, 2017
   
Text Size
image image image image
Study finds weaknesses in media Coverage, provides remedies A study conducted on the performance of the media both print and electronic in the country has established weaknesses in news gathering techniques, sourcing, balancing and comprehensiveness of information.
Govt urged to increase efforts to find missing journalist   With the disappearance of Azory Gwanda, a journalist reporting for Mwananchi newspaper entering the third week with no sign of his whereabouts, the Media Council of Tanzania (MCT) and four other civic organizations have strongly appealed to the Government to double efforts to find the missing scribe.
Four civic organizations to hold joint press conference on missing journalist   Four civic organizations will hold a joint press conference on Saturday December 9, 2017, following the disappearance of a journalist working for Mwananchi newspaper, Azory Gwanda.
MCT pleads with security organs to safely deliver missing journalist The Media Council of Tanzania (MCT) has urged security organs to ensure that journalist Azory Gwanda who is reported to have disappeared for over two weeks is found safe and sound.

ZA KISWAHILI

Resource Centre

IRC1

Press Clippings

Media Council of Tanzania Website

kajubiimpunity2017

Baraza la Habari Tanzania (MCT) limeeleza wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa jinai dhidi ya wanahabari nchini.

Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga amesema Baraza haliridhiki na hali ya uhuru wa habari nchini.

Alikuwa akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupinga Jinai Dhidi ya Wanahabari Novemba 2, kama ilivyopitishwa na Umoja wa Mataifa katika kikao chake cha 68 kilichofanyika mwaka 2013.

Alisema” siku hii ni muhimu kwa wanahabari nchini kwa kuwa inatukumbusha kwamba kuna maeneo ambapo kazi yetu haipendwi... ikimaanisha kuwa ni hatari ”.

“Inatukumbusha sote dhamira ya kufanya kazi yetu. Tunaahidi na kuthibitisha dhamira yetu.. ni kazi yetu na tutaifanya na hatutayumbishwa kwa kuwa tunapinga kabisa jinai  dhidi ya kutoshughulikiwa kwa madhila yanayowapata waandishi”, Mukajanga alisema.

Alitaja matukio kadhaa hapa nchini ambapo wanahabari walifanyiwa jinai bila wahusika kuchukuliwa hatua.

Alisema mkosaji mkuu wa jinai dhidi ya wanahabari ni serikali kwa kupitia, polisi ,wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa na hata Wizara ya Habari ambayo imeshitakiwa na magazeti kadhaa ambayo wizara hiyo imeyafungia.

Kutokana na kukosa uvumilivu utawala wa sasa katika kipindi hiki kifupi imeyafungia magazeti matano- - Mseto, Mwanahalisi, Mawio, Tanzania Daima na Raia Mwema.

mediaimpunity2017

Mukajanga katika taarifa yake amempongeza Mwneyekitki wa Kamati ya Mahesabu ya Bunge , Naghenjwa Kaboyoka, kwa kukemea polisi kwa kumkamata kwa muda mwandishi wa Nipashe Dodoma, Augusta Njonji, kwa kuandika habari za kikao cha kamati hiyo.

Mwandishi huyo alikuwa anafanya kazi yake, alisema Mukajanga na kuongeza kuwa hatua hiyo ni ya kupongezwa sana kwa kuwa imeonyesha mhimili mmoja wa dola unaheshimu kazi inayofanywa na waandishi wa habari katika jamii.

Katika miaka miwili, alisema , woga unaongezeka kila siku kwa waandishi wa habari na tasnia ya habari na kuwafanya washindwe kufanya kazi kwa uhuru na weledi.

Matumizi mabaya ya madaraka, upindishaji wa sheria, unyanyasaji, na ujahili na hata kutolewa kauli za vitisho na viongozi yakiambatana na ari kubwa ya kufungia vyombo vya habari kwa kiasi ambacho hakijawahi kuonekana katika historia ya Tanzania, ni mambo yanayolishushia hadhi taifa mbele ya jumuiya ya kimataifa.

Aliwataka waandishi kuitumia kwa ukamilifu na kuripoti katika rejista ya ukiukaji wa uhuru wa vyombo vya habari inayosimamiwa na Baraza la Habari tangu mwaka 2012 matukio yote ya ukiukaji wa uhuru wa habari yanayowakabili katika utekelezaji wa majukumu yao.

Alisema pia kuanzia sasa Baraza litafikisha mahakamani matukio yote ya uvunjifu wa uhuru wa habari na kuwataka waandishi   kurikodi kwa umakini matukio yote ya ukiukaji wa uhuru wa habari.

Pia aliwataka wahariri na waandishi kuzingatia kwa weledi wa hali ya juu sheria zote za habari katika ukusanyaji na uchakataji wa habari mbalimbali.

Kuhusu sheria alisema ingawa zinaweza kuonekana kuwa mbaya, lakini ndizo zilizopo na kwamba serikali inaweza kuzitumia wakati wowote.

Alisema Baraza linahimiza jitihada za pamoja kuhakikisha sheria hizi mbaya zinafutwa ama zinafanyiwa marekebisho.

Mukajanga pia alisema kwa kuzingatia kwa dhati weledi na maadili ndiyo ulinzi wa kwanza dhidi ya wale wanaotaka kupoka haki na uhuru wa habari.

Media Headlines

MCT Videos
videoMore Videos...

Photo Gallery
photoMore Photos...

Journalism Awards

awaa

Visitors Counter

2416957
Today
All days
840
2416957

OUR RSS

  • No feeds found!