Monday, January 22, 2018
   
Text Size
image image image image
UNESCO/Guillermo Cano World Press Freedom Prize Click the link below for more information and nomination form for 2018 https://mct.or.tz/index.php/unesco-prize
MCT participates in Boresha Habari project The Media Council of Tanzania ( MCT) is participating in a major project that seeks to support an open and inclusive environment in which media and civil society provide accurate and impartial information.
Christmas and New Year
Study finds weaknesses in media Coverage, provides remedies A study conducted on the performance of the media both print and electronic in the country has established weaknesses in news gathering techniques, sourcing, balancing and comprehensiveness of information.

ZA KISWAHILI

  • 1
  • 2
  • 3
  • 4

Resource Centre

IRC1

Press Clippings

Media Council of Tanzania Website

Azory Gwanda mwandishi wa gazeti Manwanchi aliyetoweka kutoka kituo chake cha kazi Kibiti Mkoa wa Pwani kwa karibu wiki tatu sasa ni mzaliwa wa Kigoma, Tanzania na ana umri wa miaka 42.

Alipata elimu yake ya Msingi huko Kigoma katika shule ya Msingi Msimba kisha kuhamia shule ya Msingi Bulangamilwa iliyopo Tabora na baadae kujiunga na elimu ya sekondari katika shule ya Sekondari ya Nanga iliyopo Igunga mkoani Tabora na baadaekuhamia Dar es Salaam kwa kaka yake miaka ya 90.

Alisoma kozi mbali mbali fupi na ndefu ikiwa ni pamoja na kusomea Uandishi wa Habari na kupata Stashahada katika Chuo cha Maarifa kilichopo Jijini Dar es Salaam.

Amekuwa mwandishi wa kujitegemea hadi pale alipojiunga na Kampuni ya Mwananchi ambapo pia anafanya kazi kama mwandishi binafsi kwa gazeti la Mwananchi katika Wilaya ya Kibiti Mkoa wa Pwani.

Azory Gwanda pia aliwahi kufanya kazi katika kituo cha Redio cha WAPO FM kama mwandishi mwandamizi.

Katika miaka ya 2016 na 2017, yalitokea machafuko na mauaji makubwa yaliyokuwa yakiratibiwa na watu wasiojulikana katika wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani ambapo Gwanda anapoishi na kufanya kazi za uandishi wa habari.

Kwa mujibu wa Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, kila mtu ana haki ya kupata na kutoa habari. Tafsiri ya Ibara hii haijamtenga Mwandishi wa Habari kwakuwa naye ni raia kama raia wengine wanaozungumziwa katika Katiba yetu hususani Ibara tajwa hapo juu.

Hivyo kwa mazingira hayo mwandishi asingetemewa aache kazi yake ya kutoa habari kwani ana haki Kikatiba. Taarifa zinaonyesha Gwanda alikuwa mstari wa mbele katika kuandika taarifa za mbalimbali za ukiukwaji wa haki, mauaji na matukio yanayotokana na hali ya Kibiti kiusalama.

Gwanda kama mwandishi amekuwa akitumia haki hiyo kuweza kutoa habari mbalimbali juu ya kile kilichokuwa kinatokea Wilayani Kibiti.

Hata baada ya mapigano kupungua aliendelea kutafuta habari na kuufahamisha umma kwani zilisambaa habari kwamba bado kuna mauaji ya chini chini bado yanaendelea katika Wilaya hiyo, hivyo kwake bado alikuwa na jukumu la kufanya utafiti na kuweza kuuhabarisha umma wa Watanzania kupitia gazieti la Mwananchi.

Ni kwa mazingira hayo ambayo tunadhani huenda yamepelekea usalama wake kuwa hatarini.( Ripoti na Florid Mapunda)

Media Headlines

MCT Videos
videoMore Videos...

Photo Gallery
photoMore Photos...

Journalism Awards

awaa

Visitors Counter

2448082
Today
All days
423
2448082

OUR RSS

  • No feeds found!