Monday, January 22, 2018
   
Text Size

ZA KISWAHILI

  • 1
  • 2
  • 3
  • 4

Articles

MCT yampongeza Nnauye

nape

Nape Nnauye, Katibu Mwenenzi wa chama tawala – CCM, ndiye Waziri mpya wa habari.

Ametajwa kwenye Baraza jipya la Mawaziri lililotangazwa na Rais John Pombe Magufuli Desemba 10, 2015.

Akizungumzia uteuzi wa Waziri huyo mpya Waziri wa Habari, Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania, Kajubi Mukajanga amempongeza Nnauye na kueleza utayari wa Baraza kufanyakazi naye.

Pia alieleza matumaini kwamba waziri huyo mpya ataharakisha mchakato wa kupitishwa kwa sheria mpya za habari.

Sheria hizo mpya – Sheria ya Haki ya Kupata Habari ilizuiwa katika ngazi ya Kamati ya Bunge mwaka huu ili kuwezesha kupatikana kwa maoni ya wananchi ambapo mapendekezo ya sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari hayakufikia ngazi hiyo.

“ Tunaweka matumaini yetu kwake kutokana nguvu yake ya ujana, ataupa msukumo mchakato wa kupitishwa kwa sheria hizo ndani ya kipindi cha mwaka mmoja”, Mukajanga alisema.

Journalism Awards

awaa

OUR RSS

  • No feeds found!