Monday, January 22, 2018
   
Text Size

ZA KISWAHILI

  • 1
  • 2
  • 3
  • 4

Serikali yahimizwa kuongeza juhudi kumtafuta mwandishi aliyetoweka

thrdc

Ikiwa imeingia wiki ya tatu tangu Azory Gwanda, mwandishi wa gazeti la Mwananchi kutoweka bila kuwepo dalili za kupatikana, Baraza la Habari Tanzania (MCT) na asasi zingine nne za kiraia wameitaka serikali kuongeza juhudi za kupatikana mwandishi huyo.

Katibu Mtendaji wa The MCT , Kajubi Mukajanga, akisoma taarifa ya pamoja mbele ya waandishi wa habari kwenye ofisi za Baraza Desemba 9, 2017 amesema serikali ihakiklishe inawakamata na kuwachukulia hatua za kisheria wote waliohusika na kutoweka kwa Gwanda ikiwa ni hatua ya kukomesha utekajio nyara.

Katika taarifa hiyo MCT , Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari (UTPC) na Umoja wa Waandishi wa Kupambana na Dawa za Kulevywa Tanzania (OJADACT) wameeleza wasiwasi mkubwa kutokana na kuongezeka kwa vitendo vya watu kutoweka nchini.

Kudhibiti hali hiyo, asasi hizo tano zimewataka watetezi wa haki za binadamu kutoa sauti kwa pamoja dhidi ya kutoweka watu kunakoongezeka kwa kasi.

Pia wameitaka serikali kusaini na kuridhia miktaba ya kimataifa ya kulinda watu waliotekwa na waliowekwa kizuizini na pia kusaini makubaliano ya kimataifa dhidi ya utesaji na vitendo vingine vya kikatili vinavyotweza utu wa Binadamu..

Bunge limetakiwa kujadili suala la watu kutoweka na kutoa maazimio.

Vyombo vya habari kwa upande wao vimetakiwa kuendelea kuchunguza na kuhabarisha umma ambao kwa upande wake umetakiwa kuwafichua watu wenye nia ovu ya kuwadhuru watanzania wenzao.

Kuhusu uhuru wa kujieleza taarifa hiyo imetoa mwito kwa mashirika ya kimataifa kuwaunga mkono watanzania kupinga hatua za kubinya uhuru na haki ya kupata habari.

Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) inayochapisha magazeti ya Citizen na Mwananchi imepongezwa kwa kuwa mstari wa mbele katika jitihada za kumtafuta mwandishi wake aliyetoweka Gwanda.

Kampuni hiyo imeelezwa kuwa ni mfano kwa makampuni mengine ya habari kwa kuonyesha wasiwasi na juhudi inazochukua kumtafuta mwandishi huyo..

Mratibu wa Taifa wa THRDC, Onesmo ole Ngurumwa alisema wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari uliohudhuriwa pia na Mkurugenzi Mtendaji wa MCL, Francis Nanai , kuwa walipeleka timu ya uchunguzi kupata ukweli wa mambo Kibiti.

Katika uchunguzi wao alisema, timu hiyo ilimhoji mke wa Gwanda, majirani, viongozi wa serikali ya mtaa na Polisi.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, Theophile Makunga pia alihudhuria mkutano huo wa waandishi wa habari.

Journalism Awards

awaa

OUR RSS

  • No feeds found!