Saturday, February 17, 2018
   
Text Size

Wadau wa habari wajadili kesi dhidi ya sheria mpya ya habari

ligationjan2018

Wawakilishi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) wamekuwa na mkutano na wanasheria kuzungumzia maendeleo ya kesi iliyofunguliwa kupinga baadhi ya vipengele vya Sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari ya 2016.

Kesi hiyo ilifunguliwa katika Mahakama Kuu Mwanza . Mkutano huo pia ulijadili kuhusu kesi ya kikatiba dhidi ya vipengele vya sheria hiyo iliyofunguliwa katika Mahakama ya Afrika Mashariki, mjini Arusha.

Mkutano huo uliofanyika katika ofisi za MCT, pia ulizungumzia hatua ya karibuni ya Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Udhibiti Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuvitoza faini ya jumla sh. Milioni 60 vituo vitano vya Televisheni kwa kukiuka vifungu vya kanuni za utangazaji.

Vituo vilivyotozwa faini ni ITV, Azam, Star, EATV na Channel Ten.

Journalism Awards

awaa

OUR RSS

  • No feeds found!