Tuesday, February 20, 2018
   
Text Size

Kanuni za maudhui ya mtandaoni zinabana uhuru wa kujieleza - MCT

kajubingc2017

Rasimu ya mapendekezo ya Kanuni za Maudhui ya Mitandaoni na Mawasilano ya Posta iliyochapishwa na Serikali inabana uhuru wa kujieleza na uhuru wa vyombo vya habari.

Pia zinabana uhuru wa uhariri ambao ni nguzo kuu na ya msngi ya uandishi wa habari.

Haya yameelezwa katika uchambuzi wa rasimu hiyo uliofanywa na Baraza la Habari Tanzania(MCT).

Baraza limeeleza kuwa wakati iliichukua serikali miaka saba kuibuka na rasimu hiyo ya kanuni za maudhui ya mtandaoni, yenyewe iliitisha mkutano kwa taarifa ya muda mfupi kuwataka wadau kutoa maoni yao katika muda wa siku mbili tu.

 Wadau wachache waliofanikiwa kuhudhuria mkutano uliotishwa na serikali katika ukumbi wa kituo cha kimataifa cha mikutano cha Julius Nyerere mjini Dar es Salaam Septemba 28, 2017 waliomba muda zaidi kuweza kutoa maoni yao.

 Serikali iliwataka kutoa maoni yao ndani ya siku mbili katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyoitoa kuitisha mkutano huo Septemba 26, 2017.

 Kufuatia maombi ya wadau serikali ilikubali na kuahirisha muda wa kutoa maoni hadi Oktoba 6, 2017.

 Kwa kuwa serikali ilichukua miaka saba kuandaa rasimu ya Kanuni hizo, kwa hakika ingeweza pia kutoa muda zaidi kwa wadau kutoa maoni yao.

 Kulingana na uchambuizi wa MCT, vifungu vya Kanuni hizo   havikidhi viwango vya eneo na vya kimataifa kuhusu haki ya uhuru wa kujieleza kwenye Intaneti. “Pia havikidhi viwango vya kikatiba kama ilivyo kwenye kifungu cha 18 cha Katiba,”, uchambuzi huo umeonyesha.

 Hivyo imependekezwa na MCT wadau wahimize kuwepo mabadiliko ya kanuni hizo au yafunguliwe mapitio ya kisheria ya uhalali wa Kanuni hizi katika Mahakama Kuu ya Tanzania ama   vyombo vingine vya juu katika nchi za eneo hili.

Journalism Awards

awaa

OUR RSS

  • No feeds found!