Reginald Mengi afariki
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, hayati Reginald Mengi , akishaurina jambo na Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania, Kajubi Mukajanga, wakati wa sherehe za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2015. Kulia ni aliyekuwa mgeni rasmi wa EJAT, Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala , Bahome Nyanduga.
Mmiliki mkubwa wa vyombo vya habari Tanzania, Reginald Mengi, amefariki. Taarifa ya kifo chake ilitangazwa mapema Alhamisi Mei 2,2019 na vyombo vyake vya habari – Radio One na kituo cha runinga cha ITV.
Watangazaji wa vituo hivyo walisoma taarifa fupi: Tunasikitika kutangaza kifo cha Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi kilichotokea Dubai usiku uliopita.Mungu aiweke roho ya Mwenyekiti peponi.
Haabari hiyo haikuwa na maelezo zaidi.
Mengi amekuwa mtu muhimu katika vyombo vya habari vya Tanzania akimiliki magazeti makubwa ya– The Guardian na Nipashe.
Pia alimiliki kituo cha runinga cha Indrependent Televisison na chaneli kadhaa ikiwa pamoja na Capital TV na East Africa TV.
Alianzisha biashara zake za vyombo vya habari mapema miaka ya 90 kufuatia sera ya kiuchumi ya kiliberali iliyoanzishwa na Rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi.
Wafanyabiashara wengine waliingia kwenye biashara ya vyombo vya habari kwa kuanzisha vyombo vipya ama kwa kununua vilivyokuwepo kama kampuni ya New Habari na Azam Media
Mengi alikuwa Mwenyekiti mwaznislishi wa wa Chama cha Wamiliki wa Vyo mbo vya Habari Tanzania (MOAT) nafasi aliyosbhikilia hadi alipofikwa na umauti.
Jina la mengi ni maarufu katika jamii kutokana na desturi yake ya kusaidia watu wenye changamoto kimaisha katika jamii.