Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2019, Kajubi Mukajanga,akizungumza wakati wa kutangaza wateule ya Tuzo hizo. Kushoto ni Meneja Programu wa MCT, David Mbulumi.
Kamati ya Maandalizi ya Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari (EJAT) kwa mwaka 2019 imetangaza majina ya wateule 54 wanaowania tuzo hizo katika makundi 21.
Wateule hawa wametangazwaSeptemba 17, 2020 baada ya Jopo la Majaji lililokutana Jijini Dar es Salaam kuanzia Septemba 08 hadi 14, 2020 kumaliza jukumu la kupitia kazi zilizowasilishwa kuwania tuzo hizo.
Kati ya wateuliwa hao 25 ni kutoka magazeti, tisa kutoka redio , wanne kutoka runinga, Kati ya wateule hao, 24 ni wanawake – saba wakiwa wanatoka kutoka kwenye magazeti, mmoja kwenye vyombo vya habari vya mitandaoni na 16 kutoka vyombo vya kieletroniki wakati wateule wanaume ni 30 ambapo 17 kati yao ni wa magazeti na wanane ni wa vyombo vya eletroniki na wanne wa vyombo vya habari vya mitandaoni.
Jopo la Majaji liliongozwa na Pudenciana Temba. Majaji wengine ni Mohammed Kissengo, Imane Duwe, Khalfan Said, Mkumbwa Ally na Pili Mtambalike ambaye alikuwa katibu wa jopo hilo.
Washindi wa tuzo hizo watajulikana rasmi katika kilele cha Tuzo za EJAT kitakachokuwa Septemba 28,2020 katika hoteli ya Tanga Beach Resort, mjini Tanga ambapo mgeni rasmi atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mheshimiwa Martin Shigela.
Jumla ya kazi 450 ziliwasilishwa kwa EJAT 2019. Kati ya hizo 192 ni kutoka magazeti wakati wanahabari wa redio na ruinnga waliwasilishwa kazi 250 na vyombo vya habari vya mitandaoni kazi nane.
Taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Maandalizi ya EJAT, Kajubi Mukajanga imeeleza kuwa kwa waandaji wa EJAT – Baraza la Habari Tanzania na washirika , mwelekeo huu ni mzuri licha ya matatizo yaliyokuwepo kwa kuwa wanahabari wengi zaidi wanaenzi na kuthamani EJAT, ambayo safari hii ni ya mwaka wa 11, kama kipimo muhimu kwa umahiri wa uandishi wa habari.
Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya EJAT ni Baraza la Habari Tanzania ambalo ni Mwenyekiti, Wakfu wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF), Taasisi yaHhabari ya Kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (MISA-Tan), Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), HakiElimu, ANSAF, Umoja wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) na SIKIKA.
Ifuatayo ni orodha ya wateule kutoka vyombombali vya habari
WATEULE WA EJAT 2019
SN | JINA LA MTEULE
|
CHOMBO HA HABARI | MKOA |
1 | Neema Goyayi | AFM Radio | Dodoma |
2 | Fatma Abdallah Chikawe | AZAM TV | Dar es Salaam |
3 | Amina Semagogwa | Radio Kwizera | Kagera |
4 | Sauli Gilliard | Daily News | Dar es Salaam |
5 | Editha Karlo | Mtanzania | Kigoma |
6. | Zuhura Juma Said | Zanzibar Leo | Zanzibar |
7 | Idi Juma | Afya Radio | Mwanza |
8 | Yohani Gwangway | Radio SAUT | Mwanza |
9 | Dominic Mrimi | Radio SAUT | Mwanza |
10. | Gwamaka Alipipi | Nipashe | Dar es Salaam |
11 | Halili Letea | The Citizen | Dar es Salaam |
12. | Alfred Lastek Mushi | Habari Leo | Dar es Salaam |
13. | Sanula Athanas Sanula | Nipashe | Dar es Salaam |
14 | Baraka Jailosi Messa | Habari Leo | Songwe |
15. | Asha Ahmed Omar | Chuchu FM | Zanzibar |
16 | Hilda Phoya | Mlimani TV | Dar es Salaam |
17 | Agnes J. Almasy | ITV | Dar es Salaam |
18 | Deogratias Damian Macha | Fountain Radio | Kilimanjaro |
19 | Kelvin Matandiko | Mwananchi | Dar es Salaam |
20. | Kareny Masasy | Habari Leo | Shinyanga |
21 | Evanc Ng’ingo | Habari Leo | Dar es Salaam |
22 | Anord Jovine Kailembo | Radio Kwizera | Kagera |
23 | Agnes Mbapu | TBC1 | Dar es Salaam |
24 | Adella Herry Tillya | EFM Radio | Dar es Salaam |
25 | Betty Tesha | TBC Taifa | Dar es Salaam |
26 | Khamis Suleiman Said | Channel 10 | Dar es Salaam |
27 | Jamaly Hashim Said | Azam TV | Dar es Salaam |
28 | Essau Kalukubila | Radio Jamii Micheweni | Pemba |
29 | Joseline Joseph Kitakwa | TBC FM | Dar es Salaam |
30 | Isidory Peter Mtunda | Pambazuko FM | Ifakara, Morogoro |
31 | Ashton Balaigwa | Nipashe | Morogoro |
32 | Faraja Sendegeya | Azam TV | Dar es Salaam |
33 | Adam G. Hhando | CG FM | Tabora |
34 | Kija Yunus Mohamed | Clouds TV | Dar es Salaam |
35 | Regina Kulindwa | Radio Sauti | Mwanza |
36 | Agnes Anderson | AFM Radio | Dodoma |
37 | Rehema Mwaikema | Azam TV | Mwanza |
38 | Husna Mohammed Khamis | Zanzibar Leo | Zanzibar |
39 | Rehema Goodluck | Mwananchi | Dar es Salaam |
40 | Lucas Raphael | Habari Leo | Tabora |
41 | Marco Maduhu | Nipashe | Shinyanga |
42 | Sifa Lubasi | Habari Leo | Dodoma |
43 | Harriet Makweta | Mwananchi | Dar es Salaam |
44 | Godfrey Kahango | Mwananchi | Dar es Salaam |
45 | Rahma S. Ali | Zanzibar Leo | Zanzibar |
46 | James Kandoya | The Guardian | Dar es Salaam |
47 | James Kamala | Daily News | Dar es Salaam |
48 | Crispin Samson | The Guardian | Dar es Salaam |
49 | Hadija Omar Nassor | Voice of Tabora | Tabora |
50 | Aurelia Palali | Kwizera radio | Kagera |
51 | Abdul Kingo | Nipashe | Dar es Salaam |
52 | Muhidin Msamba | The Guardian | Dar es Salaam |
53 | Bakar Masoud Bakar | Chuchu FM | Zanzibar |
54 | Rajab Mustapha Mrope | Pangani FM | Pangani, Tanga |
Makundi yaliyoshindaniwa ni :
- Tuzo ya Kuripoti Biashara Uchumi na Fedha
- Tuzo ya kuripoti Utamaduni na Michezo
- Tuzo ya Kuripoti Kilimo na Biashara ya Kilimo
- Tuzo ya Kuripoti Elimu
- Tuzo ya Kuripoti Utalii na Uhifadhi
- Tuzo ya Kuripoti Habari za Uchunguzi
- Tuzo ya Uandishi Habari wa Data
- Tuzo ya Kuripoti Haki za Bianadamu na Utawala Bora
- Tuzo ya Mpiga Picha Bora
- Tuzo ya Mpiga Picha Bora wa Runinga
- Tuzo ya Mchora Vibonzo Bora
- Tuzo ya Kuripoti Jinsia
- Tuzo ya Kuripoti Wazee
- Tuzo ya Kuripoti Watoto
- Tuzo ya Kuripoti Usimamizi wa Mafuta, Gesi na Uchimbaji Madini
- Tuzo ya Kuripoti Afya ya Uzazi
- Tuzo ya Kuripoti Ubunifu wa Maendeleo ya Binadamu
- Tuzo ya Kuripoti Athari za Kemikali kwa Afya na Mazingira
- Tuzo ya Kuripoti Usalama Barabarani
- Tuzo ya Kuripoti Hedhi Salama
- Tuzo ya Wazi