Jaji Makaramba ahimiza mawakili kutetea haki, uhuru wa kujieleza

Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Baraza  la Habari (MCT) Jaji  Robert Makaramba akizungumza katika mafunzo ya  mawakili iliyoandaliwa na Baraza mjini Zanzibar.

 

Jaji Makaramba ahimiza mawakili kutetea haki, uhuru wa kujieleza

Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Baraza la Habari Tanzania, Jaji mstaafu Robert Makaramba  amewaambia mawakili waliohudhuria mafunzo ya sheria yaliyoandaliwa na Baraza kuwa  wao ni muhimu  kwa kutetea haki ya uhuru wa kujieleza.

Aliwaambia washiriki  hao kuwa mafunzo hayo ya siku tatu yaibue ari ya kusaidia katika maeneo  hayo kwa wanahabari, vyombo vya habari na  kwa jamii nzima.

Naye  Wakili  Mwandamizi Mpale Mpoki alisema wakati wa mafunzo hayo kuwa ni muhimu  zaidi kuzuia vipengele kandamizi kuliko kusubiri kuvipinga mahakamani na kwingineko.

Aliwaambia mawakili hao kuwa  wanatakiwa  kushiriki kikamilifu  kwenye mchakato ya utungwaji wa sheria mbalimbali.

“Tumieni  nafasi zinazotolewa kupeleka maoni ya kupata sheria bora”, wakili Mpoki alisema.

Naye Meneja Programu wa  Mpango wa kusaidia vyombo vya habari  (IMS), Fausta Musokwa amesema  kuna uhitaji  mkubwa wa utetezi  wa kisheria kwa waandishi wa habari na kwamba yapo mazingira ambapo  mwandishi ama chombo  anajikuta  katika eneo lake na hakuna aliye karibu.

Musokwa alisema amewashukuru  mawakili hao  kwa utayari wao  kusaidia eneo hilo wakati mwingine hata kwa ushauri tu wa namna salama ya kujiendesha.