Wanahabari 60 wateuliwa kuwania Tuzo EJAT 2021

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2021, Kajubi Mukajanga akitaja majina ya wateule wa EJAT) 2021 mbele ya Waandishi wa Habari
Wanahabari 60 wameteuliwa kuwania Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2021
Majina ya wateule hao yalitangazwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya EJAT, Kajubi Mukajanga kwenye mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika Mei 19, 2022.
Mshindi wa jumla na washindi wa makundi mengine ya mashindano hayo watafahamika katika kilele chake kitakachofanyika katika hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam Mei 28,2022.
Rais Samia Suluhu Hassan atakuwa mgeni rasmi wa Tuzo hizo. Atawapa Tuzo na zawadi kwa mshindi wa Jumla na mshindi wa Tuzo ya Mafanikio ya Maisha ya Uandishi wa Habari (LAJA) kwa mwaka 2022.
Hii ni mara ya 13 mashindano hayo ya kila mwaka ya kuwatuza wanahabari kwa kufanyakazi nzuri. Mashindano ya kwanza yalifanyika mwaka 2009.
Rais Suluhu anakuwa Rais wa pili aliyeko madarakani kuwa mgeni rasmi katika mashindano hayo. Rais wa kwanza alikuwa Jakaya Kikwete aliyekuwa mgeni rasmi wa EJAT 2011.
Wateule hao na majina ya vyombo vyao vya habari katika mabano ni kama ifuatavyo:- Mariam Shabani Mbwana (Mwananchi;Tumaini Godwin Msowoya (Mwananchi); Peter Simon Rodgers (ITV);Agusta Mathias Njonji (Nipashe); Nusra Shaaban Kichonapishi (TIFU TV-Online);Adam Gabriel Hhando (CG FM radio);Haji Nassor Mohamed (Zanzibar Leo);Khamisuu Abdallah Ali (Zanzibar Leo); Naishooki Alais Makaseni (Star TV) na Sanula Renatus Athanas (Nipashe).
Wengine ni Lugendo Ibrahim Madege (UFM Radio);Anthony Mayunga Mayunga (Mwananchi); Ephrahim Edward Bahemu(Mwananchi); Maryam Salum Habib (Zanzibar Leo); Said Seleman Lufune (City FM); Paschal Michael Buyaga (TBC1); Aurea Simtoe (Mwananchi); Salum Vuai Issa (Zanzibar Leo);Masekepa Natisa Masekepa (ITV), Sabato Mafwiri Kasioka (Nipashe);Muhidin Ally Msamba (The Guardian) Amina Ahmed Mohamed(Zanzibar Leo ) na Harith Jaha Ally (watetezi TV- Online);
Pia kwenye orodha ya wateule wamo Gladness Joseph Mseti (UFM Radio);Zuhura Hassan Makuka (Dar 24 Online); Jackline Inyas Silem (ITV); Francis Dhamira Kajubi (The Guardian); Isakwisa Njole Mbyale ( Highlands FM Radio); Harieth Isaya Makweta (Mwananchi); Halfan Chusi (Nipashe); Khalifa Said Rashid (The Chanzo – Online); Irene Nicholaus Mwasomola ( (Uhuru); Elibeth Edward Kusekwa (Mwananchi; Baraka Jailos Messa (Habari Leo); Martha Stephen Nalimi (Shamba FM); Joyce David Joliga (The Citizen); Mariam Ngollo John (Nutka. Blog) na Najjat Haji Omar(The Citizen).
Wengine ni Salma Msichoke Mrisho(Star TV); Peter Lugendo John (TBC FM), Beatrice Philemon Mukocho (The Guradian); Joe Beda Rupia (Jamhuri), Hanifa Salim Mohamed (Zanzibar Leo);Amour Khamis Ali (Zanzibar Cable TV); Abdi Juma Seleman (Zanzibar Leo); Protte Profit Mmanga (LEO TV-Online); Faraja Sendegeya (Azam TV); Festo Charles Lumwe ( Dar 24 – Online) na Mary Geofrey Mashina (Nipashe).
Wengine ni Munira Abdillah Hussein (BBC Swahili Online); Daniel Samson ( Nukta.habari blog); Habiba Zarali Rukuni (Zanzibar Leo)Marco Zephania Maduhu (Nipashe); Christina Stephen Mwakangale (The Guardian); Elizabeth Corney Zaya( Nipashe); Sudi Shaban Ally ( Star TV); Omary Huzssein Omary (Star TV); Jecha Simai Jecdha (ZBC FM); Jenifer Julius Gilla ( The Guardian) na Lukelo Francis Haule ( The Chanzo- Online).
Wateule hao waliteuliwa na jopo la majaji saba lililoongozwa na Mhariri Mkongwe Mkumbwa Ally. Majaji wengine katika jopo hilo ni Mwanzo Millinga aliyekuwa Katibu Aboubakar Famau, Mbaraka Islam, Imane Duwe, Beatrice Bandawe na Rose Haji.
Majaji walianza kupitia kazi 598 zilizowasilishwa kuwania tuzo Mei 7 na wakamaliza Mei 15.
EJAT 2021 ina makundi 20 ambayo ni Uchumi, Biashara na Fedha; Michezo na Utamaduni; Kilimo na Biashara ya Kilimo; Elimu; Utalii na Uhifadhi ; Habari za Uchunguzi; Uandishi wa Data; Haki za Binadamu; Haki za Binadamu na Uwajibikaji; Mpiga Picha Bora – Magazeti, Mpiga Picha Bora Runinga na Mchora Vibonzo Bora .
Makundi mengine ni Tuzo ya kuripoti Watoto; Kuripoti Watu wenye Ulemavu; Afya; Sayansi na Teknolojia, Hedhi Salama, Ushirika na Kundi la Wazi.
Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya EJAT ni Baraza la Habari Tanzania (MCT), Wakfu wa Vyombo vya Habari Tanzania(TMF), Hakielimu , Agriculture Non State Actors Forum (ANSAF), Umoja wa Klabu za Uandishi wa Habari Tanzania (UTPC),Taasisi ya Habari Kusini mwa Afrika tawi la Tanzania MISA na Twaweza.
Wafadhili wa EJAT 2021 ni Wajibu Institute, Natural Resources Governance Institute (NRGI), Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC) Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Busota Inn, Hoteli ya Serena Dar es Salaam, Coca cola, Kampuni ya Bia (TBL), Azam Media, Twaweza, COSTECH, Bank ABC and Hakielimu.