Jaji Makaramba ahimiza mawakili kutetea haki, uhuru wa kujieleza

Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Baraza la Habari (MCT) Jaji Robert Makaramba akizungumza katika mafunzo ya mawakili iliyoandaliwa na Baraza mjini Zanzibar.
Jaji Makaramba ahimiza mawakili kutetea haki, uhuru wa kujieleza
Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Baraza la Habari Tanzania, Jaji mstaafu Robert Makaramba amewaambia mawakili waliohudhuria mafunzo ya sheria yaliyoandaliwa na Baraza kuwa wao ni muhimu kwa kutetea haki ya uhuru wa kujieleza.
Aliwaambia washiriki hao kuwa mafunzo hayo ya siku tatu yaibue ari ya kusaidia katika maeneo hayo kwa wanahabari, vyombo vya habari na kwa jamii nzima.
Naye Wakili Mwandamizi Mpale Mpoki alisema wakati wa mafunzo hayo kuwa ni muhimu zaidi kuzuia vipengele kandamizi kuliko kusubiri kuvipinga mahakamani na kwingineko.
Aliwaambia mawakili hao kuwa wanatakiwa kushiriki kikamilifu kwenye mchakato ya utungwaji wa sheria mbalimbali.
“Tumieni nafasi zinazotolewa kupeleka maoni ya kupata sheria bora”, wakili Mpoki alisema.
Naye Meneja Programu wa Mpango wa kusaidia vyombo vya habari (IMS), Fausta Musokwa amesema kuna uhitaji mkubwa wa utetezi wa kisheria kwa waandishi wa habari na kwamba yapo mazingira ambapo mwandishi ama chombo anajikuta katika eneo lake na hakuna aliye karibu.
Musokwa alisema amewashukuru mawakili hao kwa utayari wao kusaidia eneo hilo wakati mwingine hata kwa ushauri tu wa namna salama ya kujiendesha.