Salamu za pongezi
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amempongeza Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Ernest Sungura kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kwanza wa Mtandao wa Mabaraza Huru ya Habari Afrika (NIMCA).
Waziri Nape amesema kuwa kuchaguliwa kwa Sungura ni kielelezo cha namna Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyoshirikiana na wadau wa habari nchini katika kulinda na kutetea uhuru wa vyombo vya habari na kuahidi kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na vyombo vya habari vya ndani na vya nje ili kuhakikisha uhuru wa habari unaendelea kulindwa.