Teknolojia yavikosesha mapato vyombo vya habari vya asili - NIMCA

MOMBASA, Kenya: Mustakabali wa vyombo vya habari vya asili Afrika unakabiliwa na tishio la kukosa matangazo, kutokana na kuongezeka kwa ushawishi wa makampuni makubwa ya teknolojia kama Google, YouTube, na Instagram.

Mwenyekiti wa Mtandao wa Mabaraza Huru ya Habari Afrika (NIMCA) ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Ernest Sungura alitoa tahadhari hiyo wakati wa mkutano wa 36 wa Mwaka wa Maafisa Uhusiano na Umma Afrika (APRA 2025).

Sungura amesisitiza kuwa mabadiliko hayo ya mfumo wa matangazo, ambayo zamani yalizalisha mapato yaliyoendesha vyombo hivyo, yamehamia kwa makampuni makubwa ya teknolojia kutokana na urahisi na uharaka wake kuwafikia walaji.

Mabadiliko hayo ya kiteknolojia yamekuwa tishio kwa uendelevu na uhai wa vyombo vya habari asilia Afrika.

Mkutano wa 36 wa Mwaka wa Maafisa Uhusiano na Umma wa Barani Afrika, unaandaliwa kwa ushirikiano na Chama cha Maafisa Uhusiano na Umma Afrika (APRA) na Chama cha Mahusiano ya Umma Kenya (PRSK), umewaleta wataalamu wa mawasiliano na vyombo vya habari, maafisa wa serikali, na viongozi wa mifumo ya kidijitali kutoka ndani na nje ya Afrika. Mwisho.